Familia ya Mtoto Aliyeuliwa na Mtoto Mwenzake wa Miaka 9 Waombe Mtoto Aliyeua Aachiwe Huru


Familia ya Marehemu Ally Khalifa Bakari, Mtoto mwenye umri wa miaka tisa ambaye amefariki mara baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mwenzake hadi kupelekea kufariki Dunia, imeiomba Serikali imwachie huru Mtoto mwenye umri wa miaka tisa Mwanafunzi wa Darasa la 3 Shule ya Msingi Kichangani Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, ambaye amefanya tukio hilo, Familia hiyo inasema kilichotokea ni makosa ya kibinadamu.

Msemaji wa Familia hiyo Adriano Petro ameiambia @ayotv_ na millardayo.com kuwa ingawa Mtoto wao amefariki kilichotokea ni mapenzi ya Mungu kwakuwa Watoto hao walikuwa wakicheza pamoja siku zote na ikatokea bahati mbaya January 28 mwaka huu wakiwa wanatokea Msikitini njiani wakagombana na kupigana hadi kupelekea Ally kufariki wakati anapelekwa Hospitali.

Mariam Hassan ni Mzazi wa Mtoto anayetuhumiwa kwa mauaji (Omari Hassan ) ambapo amesema amepokea tulio hilo kwa masikitiko na kuiomba Serikali kusimamia suala la elimu kwa Mtoto wake wakati huu ambapo anashikiliwa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Hale Venusi Msonela amesema wao kama Serikali wamekaa na Familia za pande zote mbili ili kuondoa hali yoyote ya taharuki ambayo ingeweza kujitokeza.

RPC wa Tanga Sofia Jongo amesema bado Mtoto huyo anashikiliwa huku akitoa wito kwa Wazazi kutowaonesha picha ambazo haziendani na umri Watoto kwakuwa wanachojifunza hutaka kufanya kwa vitendo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad