Filamu zina nguvu sana katika suala la kumbadilisha mtu. Filamu zinaweza Jenga au kuharibu Jamii. Kuna kipindi hapo nyuma kidogo, bongo movies zilikuwa hot sana kuliko hata Bongo Fleva. Baada ya Watanzania wengi hasa Vijana kuangalia sana bongo movies walipata hasara zifuatazo.
KUAMINI KWAMBA MAISHA YA CHUO NI BATA.
Ukiangalia filamu nyingi zinazohusu maisha ya chuo, utaona wanakula bata, wakifurahi, hakuna kusoma, mapenzi kwa sana, hii imepelekea watu wengi kujua kwamba maisha ya chuo ni bata wakati sio kweli.
WANAUME WENGI KUWA MARIOO.
Filamu nyingi za kibongo hasa za Hemed unakuta mvulana wa maisha ya chini anapendwa na mdada mwenye hela, anaanza kuhudumiwa kila kitu yani ili mradi tu wakuaminishe upuuzi wakati dunia ya sasa hayo mambo hayapo, ila unakuta kijana anashinda Gym ili avutie suger mamies.
WANAUME KUIGA UPUMBAVU.
Filamu zimesababisha wanaume wengi wa Dar Kuiga kujichubua na kuvaa hereni baada ya kuwaona Mastaa Fulani wanafanya hivo.
WASICHANA KUVAA NUSU UCHI.
Wasichana wengi wameiga kuvaa vinguo vifupi kutoka kwa Wema Sepetu, Wolper, Uwoya, Aunt Ezekiel, nakadharika.
KUAMINI WAGANGA WA KIENYEJI.
Kwenye Filamu za kibongo kila shida inapelekwa kwa mganga wa kienyeji, katika filamu kumi basi tisa lazima ziwe na mganga wa kienyeji, hii imepelekea watu wengi kuamini na kuwatumia waganga wa kienyeji.
KUAMINISHA WATU KUWA DAR NDIO SEHEMU YA KUTAFUTIA MAISHA.
Filamu nyingi unakuta mtu anatoka mkoani anakuja dar kutafuta maisha, hii imefanya watu wengi sana kuiga na kuja kiholela Dar na kuishia kuangukia pua.
Endelea kutililika vitu ambavyo unahisi Ni vibaya na vimesababishwa na bongo Movies
By @hopetygatz