Kuna Baadhi ya Watu walishituka sana baada ya kujua kwamba Rihanna amemfollow @flavianamatata, Flaviana ni mtu mkubwa sana, anajuana na Trump, Beyonce, Jay Z na Wengine Kibao. Kwahiyo sio Maajabu Rihanna kumfollow Flaviana, Soma mpaka mwisho ujue namna alivyojuana na hao watu.
Flaviana Matata ni Mtanzania ambaye ni mwanamitindo wa Kimataifa, anafanya shughuli zake hasa Marekani. Mbali na mambo ya Urembo na Mitindo, pia ni mwanaharakati wa Wa maendeleo Ya wanawake na Jamii Kwa ujumla.
Flaviana matata Amewahi kuandikwa na Jarida Maarufu la Forbes kama Mwanamitindo namba Saba Africa Kuingiza kipato kikubwa Kutokana na Fani ya Urembo na mitindo. Mrembo huyu Amewahi kuingia kwenye Top 100 ya vijana wenye ushawishi mkubwa Africa.
Mwaka 2007 Flaviana matata alishinda taji la Miss Universe Tanzania, Taji lililomfanya kwenda nchini Mexico kwaajili ya Miss Universe mwaka 2017, ambapo aliweza kufika mpaka nusu fainali na ndiye mtanzania wa kwanza kushiriki Miss Universe.
Baada ya Kushiriki Miss Universe 2007, Flaviana alikutana na Russell Simmons, huyu ni mtu ambaye alimpa connection kubwa ya kufanya kazi na kampuni kubwa za Urembo na mitindo nchi Marekani.
Russell Simmons ni Film producer na Mdau mkubwa wa sanaa nchini marekani, Kubwa zaidi ni Co-Founder Wa record Label Kubwa Duniani "Def Jam", ambapo Rihanna amewahi kuwa chini ya label hiyo kuanzia mwaka 2005 mpaka 2010, Then akachukuliwa Na Rock Nation.
So, unaona kuna connection hapo Kwamba Aliyemtafutia michongo Flaviana Pia anajuana na Rihanna na Wasanii wengine wakubwa Duniani. Hivyo kuna Uwezekano mkubwa Flaviana amejuana na rihanna kupitia Russell simmons.
Mbali na Kujuana na Rihanna, Flaviana anajuana na Donald Trump hata kabla hajawa Rais wa Marekani na kuna picha zao za pamoja. Ikumbukwe kuwa, Trump ni mdau na muwekezaji mkubwa katika Tasnia ya Urembo na mitindo so inawezekana wamejuana kupitia mitindo.
Flaviana pia anajuana na Jay Z na Beyonce, wamewahi kukutana na Wakaongea Vizuri sana Kama watu fulani hivi wanaojuana kabisa. Jay Z amewahi Kuwa Rais Wa "Def Jam" kabla ya Kufungua Roc nation mwaka 2010. So Jay Z anajuana Vizuri na Russell Simmons