Freeman Mbowe "Shahidi wa Jamhuri ni Ndugu Yangu Sina Ugomvi Naye"




MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hana ugomvi na shahidi wa Jamhuri, Innocent Mdowo (37), kwani ni ndugu yake.

Mbowe ambaye ni mshtakiwa wa nne kwenye kesi ya ugaidi inayoendelea Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam, ameeleza hayo wakati akiwasalimia watu mbalimbali waliofika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

Leo Alhamisi, Januari 20, 2022, Mbowe na wezake watatu kwenye kesi hiyo, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya, ambao waliwahi kuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mara baada ya kuingia alianza kusalimia kundi moja baada ya jingine.

Mbowe alimsalimia kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Jamhuri, Robert Kidando na Kiongozi wa Jopo Mawakili wa Utetezi, Peter Kibatala na kumuacha shahidi wa Jamuri, Innocent Ndowo, aliyekuwepo kortini.


Ndipo wafuasi wa Chadema walivyomkumbusha wakimwambia “Mwenyekiti umemsahau shahidi.” Huku wakicheka.

Baada ya wafuasi hao kutoa kauli hiyo, Mbowe alidai Inspekta Ndowo ni ndugu yake, hivyo hana ugomvi naye.

“Kidando nakuona mkuu wasalimie wenzako, Kibatala nawe nakuona. Shahidi ndugu yangu sina ugomvi naye,” amedai Mbowe. Shahidi huyo aliyekuwepo ameketi katika benchi la mahakama hiyo, hakujibu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad