Haji Manara "Coastal Union inategemea Siasa za Mpira"

 


Msemaji wa Klabu ya Young Africans Haji Manara amesema klabu hiyo inaiheshimu Coastal Union, ambayo watacheza nayo keshokutwa Jumapili (Januari 16), katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.


Manara ametoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga mapema leo Ijumaa (Januari 14), ambapo amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, na wanaamini kitafanya vizuri.


Amesema heshima ni jambo kubwa sana kwao na kwa wapinzani wanaokutana nao katika kila mchezo wa Ligi Kuu ama Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, hivyo ni jukumu lao kukamilisha hilo nje na ndani ya Uwanja.

“Tunawaheshimu sana wapinznai wetu Coastal Union, na huo umekua ni utaratibu wetu kila tunapokutana na timu yoyote katika Ligi Kuu ama Kombe la Shirikisho, kikosi chetu kimekua kikicheza kwa nidhamu kubwa na ndio maana mambo yanatunyookea.”


Katika hatua nyingine Manara amesema wanafahamu wenyeji wao Coastal Union wamekua na Siasa nyingi ndani na nje ya Uwanja, lakini msimu huu wamejipanga kuzima mipango hiyo na kuondoka na matokeo mazuri kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani.


“Tunajua Coastal Union wamekua hodari kwenye siasa nyingi za mpira, hasa hasa nje ya Uwanja, tunajua wana mbinu nyingi sana lakini tumejipanga na msimu huu tutawashngaza.” Amesema Haji Manara


Young Africans haijaifunga Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani kwa misimu saba mfululizo.


Mara ya mwisho Young Africans kupata ushindi kwenye uwanja huo, ilikuwa ni Februari 4, 2015 (Msimu wa 2014/15), iliposhinda 1-0 lililofungwa na nahodha na beki wao mahiri kwa wakati huo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 11 ya mchezo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad