Hakuna Atakayegongewa Mlango Kudaiwa Deni la Taifa




“Mnamo Oktoba 10 , 2021 ulizindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 na kuelekeza fedha zote zitumike kwenye maeneo yaliyopangwa na kwa wakati.” – Mhe. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango.

“Utekelezaji wa fedha imeendelea na kuongeza imani kwa Viongozi Wakuu wa IMF na kuamua kufuta masharti yote yaliyokuwa na riba kwa upande wa fedha zenye dirisha la ‘rapid financing instrument’ ambayo ilikuwa Dola za Kimarekani milioni 378.17 sawa na 2/3 ya mkopo wote.” -Mwigulu.
“Napenda kutumia fursa hii kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa mkopo wote wa Dola za Kimarekani 567.25 sawa na Trilioni 1.3 utakuwa mkopo usio na riba kabisa” – Mhe. Mwigulu Nchemba

“Tathmini ya uhimilivu wa deni uliofanyika Novemba 2021 inaonesha deni letu ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Viashiria vinaonesha kuwa deni la serikali kwa uwiano wa pato la Taifa ni 31% ambapo ukomo wa kidunia ni 55%.”- Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

“Mkopo anapewa mwenye chanzo cha kulipa…Kwa hiyo mkopo ni biashara, tajiri na tajiri wanafanya biashara, biashara ya kutumia fedha hizo. Kwa maana hiyo, tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa uharaka.”- Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba


 
“Shirika la Fedha Duniani (IMF) limefuta masharti katika mkopo wa shilingi trilioni 1.3 na kwa maana hiyo, fedha tulizozichukua, baada ya kipindi cha mpito kupita tutazirudisha hizo hizo sh trilioni 1.3.” Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchembe.
“Mhe. Rais wale wasiotambua kuwa unafungua uchumi ili watoto wao wapate ajira wataendelea kuyaelewa haya unayofanya siku ukifungua uchumi, biashara zikakua watoto wao wakapata ajira.

“Watu wengine wakisikia neno mkopo wanashtuka, Mkopo sio Msaada, Mkopo anapewa mwenye chanzo cha kulipa , Maskini ambaye hana cha kulipa hapewi Mkopo..Kwa hiyo mkopo ni biashara, tajiri na tajiri wanafanya biashara, biashara ya kutumia fedha hizo.

“Kwa maana hiyo, tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa uharaka,” Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba
“Tutaendelea kukopa ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Tathimini ya uhumilivu wa deni tulioufanya, inaonesha ni himilivu.” – Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.


“Shilingi bilioni 28.7 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 25 vya VETA vya Wilaya na shilingi bilioni 19 ni kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo vinne vya VETA ngazi ya Mkoa ikiwemo Njombe, Simiyu, Geita na Rukwa.” – Dkt. Mwigulu Nchemba.
“Mkopo wa serikali yako wa kwanza ni huu wa trilioni 1.3 ambao hauna riba, mikopo mengine ya serikali ni ile ya Banki ya Dunia ambayo imesainiwa siku nyingi na ulipaji wake ni hadi pale itakapoiva.”- Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango.
“Hakuna siku Mtanzania mmoja mmoja atagongewa mlangoni kwake kwamba unadaiwa fedha hizi kwa sababu nchi yako ilikopa, hakuna. Pia, Marais hawakopi, ni serikali. Hili si jambo la familia, ni jambo la serikali.”- Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba
“Thamani ya sasa ya deni la nje kwa pato la Taifa ni 18.8%, ikilinganishwa na ukomo ambao ni 40%. Thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni 142%, ikilinganishwa na ukomo ambao ni 180%.”- Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

“Mpaka sasa Wizara ya Elimu imeshapokea shilingi bilioni 47.7 na kuzipeleka katika taasisi ambazo wanazisimamia ikiwemo VETA.” – Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango.
Wizara ya Elimu ilitengewa shilingi bilioni 64.9 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya ujenzi na ukarabati wa madarasa, mabweni, kumbi za miadhara, vyuo vya ualimu pamoja na maeneo ya wenye uhitaji maalumu”- Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

“Utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya mijini umeanza katika miradi 44 na mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo kukamilisha taratibu za manunuzi.” – Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Wizara ya Maji ambayo ilitengewa kiasi cha Sh bilioni 139.4, utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya vijijini hususan taratibu za manunuzi kwa miradi yote 172 zimekamilika na ujenzi upo katika hatua za awali katika baadhi ya maeneo.” – Dkt. Mwigulu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad