Harmonize Aitangaza Siku yake

 


Hatimaye mwanamuziki Harmonize ameitangaza rasmi siku ya tarehe 5 mwezi machi 2022, kuwa ndio siku rasmi ya tamasha lake kubwa ‘Afro East Carnival’ litakalofanyikia jijini Dar es salam.


Kwa mujibu wa Harmonize, tamasha hilo litawakutanisha wasanii mbalimbali kutoka katika nchini kadhaa za ukanda wa Afrika Mashariki, watakaojumuika kwa pamoja kutoa burudani kwa mashabiki wao.


“Hii inakwenda kuwa habari kubwa, wasanii wote wakubwa wa Afrika mashariki kwenye jukwaa moja, nashindwa kusubiri, ninashauku ya kujumuika na kaka na dada zangu 2/03/2022 jijini Dar es salaam.” Ameandika Harmonize.


Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Harmonize kufanikisha dhamira ya ujio wa tamasha hilo ambalo, awali halikufanikiwa kutokana na sababu alizoainisha kuwa nje ya uwezo wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad