Harmonize "Ningependa Mwaka Huu Kuona Hakuna Msanii Atakae Nunua Views Tushindane Kwa Uwazi"


#BURUDANI:Mwimbaji wa Bongofleva toka Konde Music Worldwide, Harmonize amesema kuwa kwa mwaka 2022 angependa kuona hamna msanii anayenunua views YouTube.

Harmonize amesema hayo wikiendi iliyomalizika wakati wa listening party ya albamu yake ya pili, High School.

"Mwaka wa 2022 ningependa kuona hamna msanii ambaye ananunua viewers. Wote tufanye kazi kwa bidii tuweze kusonga mbele kwa ushirikiano. Jambo hilo mzee tunatupa 2021" alisema Harmonize.

Utakumbuka kwa miaka ya hivi karibuni baadhi ya wasanii wa Bongofleva wamekuwa wakishtumiana kwa kununua views kwenye mtandao wa YouTube.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad