Ameandika Irene Uwoya kupitia page yake ya Instagram:
"Nimeona niongee, na nataka niliweke hili wazi na kila mtu aelewe since najikuta nahusishwa kutokana na ukaribu wangu na Aristote, Binafsi Nimesikitishwa sana na maneno yasiyo ya kibinaadamu yaliyotolewa na Aristote dhidi ya Wema, Watu waelewe kitu kimoja leo, Sijawahi kumtuma Aristote amtukane Wema wala mtu yeyote yule, sina ugomvi na Wema na sina sababu ya kufanya upuuzi wa namna hiyo, Nimempigia pia Aristote kuoneshwa kukasirishwa kwangu, na niseme tu hiyo ni MIHEMKO yake yeye, sihusiki na lolote juu ya hayo aliyoyaropoka ambayo yanaleta hata uchonganishi baina yetu kitu ambacho sikifurahii kwakweli, kingine nichukue nafasi hii kukupa Pole Wema kwa haya yaliyotokea, hata mimi ningekuwa wewe ningejiskia kama unavyojiskia, pole sana sana, na zaidi Aristote nathamini upendo wako kwangu lakini ningeheshimu sana kama itabaki sisi na maisha yetu bila kunilinganisha wala kunishindanisha na yeyote yule sababu mimi naishi maisha yangu siko kwenye mashindano na mtu, asanteni wote, One love!!" Irene Uwoya