Hatimaye Tundu Lissu Afunguka Spika Kujiuzulu


"Kwa miaka takribani 96 tangu kuanzishwa kwa Bunge hakujawahi kutokea ugomvi wa waziwazi kati ya Spika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeona aina hii ya ugomvi ikioneshwa mbele yetu hadharani hii ni mara ya kwanza" @TunduALissu, Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTz
-
"Kujiuzulu kwa Job Ndugai kama Spika wa @bunge_tz ni tukio la kihistoria na ni tukio kubwa kwa hostoria yetu ya kisiasa na kikatiba tangu Bunge letu lianzishwe mwaka 1926, haijawajahi kutokea Spika amelazimishwa kujiuzulu kwa namna ambayo Ndugai amelazimika kujiuzulu"@TunduALissu
-
"Kulazimishwa kwa Spika Ndugai kujiuzulu kunathibitisha wazi kabisa lile ambacho tumekisema kwa miaka mingi kwamba kwa mifumo yetu ya kikatiba na kiutawala kuwa tuna mhimili mmoja tu wa dola, na mhimili huo unaitwa Rais" @TunduALissu, Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTz
-
"Rais amekuwa na nguvu kubwa kuliko vyombo viwili vya mahakama na Bunge, ambapo katika utaratibu wa kawaida wa demokrasia vyombo vyote hivyo vinatakiwa vidhibitiane. Rais anatakiwa adhibitiwe na Bunge" @TunduALissu, Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTz
-
"Tangu mwaka 1962, utaratibu wa mihimili yetu mitatu (Bunge, mahakama na serikali) umevurugwa kwa manaa ya kwamba Rais amekuwa na madaraka makubwa sana, mamlaka yake hayana udhibiti na hawajibiki kisheria mahali popote. Anawajibika kwa Mungu pekee" @TunduALissu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad