Hii Back to Back ya Harmonize Inambomoa Badala ya Kumjenga..Wasanii Wake Haendi Ipasavyo



Ni kweli kuwa Harmonize amefanikiwa kutengeneza Fan base kubwa nchini, mashabiki wanaomsapoti kwenye kila hatua, ila cha kusikitisha ni kuwa jamaa hajafanikiwa kujitengenezea mipango yake mwenyewe ya utoaji projects zake binafsi lakini hata za Kondegang kiujumla.


kabla WCB hakujaanza kutokea mabadiliko ya kila msanii kuachia wimbo kwa muda wowote ule kama ilivyo sasa, kulikuwa na utaratibu wa jambo la fulani liende na mwingine atafwata, hii ilisaidia sana projects za WCB kwenda mbali zaidi na kila project iliyokuwa ikitoka,watu waliisubiri kwa hamu sababu ukimsikia Rayvanny au Mbosso hii leo,itakuchukua hata mwezi kumsikia tena, haikukata hamu mashabiki.


Na ilisaidia kwa wasanii kama Mbosso na Lava lava ambao ilionekana hawawezi fiti kwenye kuta za Label hiyo kuaminika, maana promotion iliyokuwa ikifanyika ilikuwa si mchezo, ikawajengea ujasiri wasanii hawa na wakaweza kusimama kwa miguu yao vizuri ndani ya Label hiyo, Leo hii wasanii hao wanaweza kufanya show zao binafsi na zikafurika,Management ya WCB inajua inacho kifanya.


Harmonize ukiacha kuwa ni msanii mwenye kipaji kikubwa, ila pia ni mkurugenzi wa Label ambayo tuliamini ingeleta ushindani kwenye huu muziki, lakini kadri siku zinavyoenda haiwi hivyo, kuna vitu anafanya kama hana Uongozi, High School ni albamu kali ambayo ilihitaji promo kubwa na muda wa kutosha ila badala yake akaanza dandia kolabo na kutelekeza albamu, Harmonize anatamani atoe ngoma kila siku na mwisho wa siku watu wanaishia kumuona wa kawaida tu, wimbo unasikilizwa siku tatu kapuni. Juzi kati kaachia video yake mpya ila leo anametuupdate matamanio yake ya kuachia wimbo, na jana kuna wimbo umetoka japo kashirikishwa. Kutoa nyimbo back to back sidhani kama itamuongezea value yake.


Kuna wasanii wanne nyuma yake,jamaa kashindwa kabisa kujinyima ili awapeleke mjini. Ana mipango mingi mizuri lakini kuna sehemu management ya Kondegang inakwama, Anahitaji/inahitaji kuwabrand wasanii wake kuliko ilivyo sasa, maana ni vipaji vilivyokosa promo tu,aige hata nusu ya maarifa kwenye uongozi wake wa zamani na sio dhambi, lasivyo...


Mfikishieni..

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad