Hii ndio Faida ya Tende Kwa Afya ya Kitandani



Matumizi ya Tende na Maziwa ni Muhimu pia vizuri sana kwa afya zetu ambapo husaidia sana kuongeza Nguvu na kuchangamsha mwili hasa katika idara ya kuleeee kitandani, Lakini pia tende ina virutubisho muhimu vinavyosaidia kupunguza nafasi ya kupata saratani yaani Kansa.
Vyakula Hivi vina virutubisho vingi ikiwemo vitamini A, B na C pia nishati au caloriesna madini kama vile magnesium, potasium, phosphorus nakadhalika, Ambapo hivi vina faida mbalimbali katika miili yetu.


Kwakweli juisi hii ya tende na maziwa ina faida nyingi mwilini ikiwemo;
1: Huongeza nguvu na ubora wa mbegu kwa wanaume hasa kwa walio na tatizo Hilo.
2: Huchochea hamu na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa kina mama Yani wanawake.
3: Kuimarisha afya ya mama wajawazito na mtoto, hii ni kwasababu huwa inaongeza damu kwa madini chuma iliyonayo na pia huongeza nguvu inayomfanya mama asiteseke wakati wa kujifungua
4: Husaidia kuondosha vilevi mwilini
5: Hukinga mwili dhidi ya saratani ya tumbo pamoja na kiharusi.

6: Husaidia mmeng’ enyo wa chakula tumboni
7: Pia huondoa tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu
8: Humuondolea mtu uchovu
9: Huongeza damu mwilini kutokana na kuwa na madini chuma kwa wingi sana
10: Husaidia mishipa ya fahamu kuwa vizuri na kufanya kazi vyema.

Kiujumla tufahamu kwamba huu mchanganyiko wa tende na maziwa ni muhimu sana kwa binadamu kwa kuwa huupa mwili lishe muhimu hivyo kuboresha afya zetu hasa za uzazi.
Baada ya Hilo pia ya tende ina protini nyingi, hivyo basi huwa faida maradufu zikitumiwa kwa kuchanganywa na maziwa ambayo pia yana protini nyingi.
Pia tende zina kiasi lehemu hivyo zinapokuwa na maziwa huwasaidia watu jinsia zote, yaani wanawake na wanaume, hasa afya ya uzazi.
Nikushauri tu usiache kutumia tende na maziwa mara kwa mara kwaajili ya afya yako.
@Ventas Malack
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad