Mshambuliaji wa zamani wa Brazil, PELE akifunga kamba viatu vyake aina ya Puma kabla ya kuanza kwa mechi ya fainali ya kombe la dunia tarehe June 21, 1970 dhidi ya Italia kwenye dimba la Estadio Azteca huko nchini Mexico.
Katika mechi hiyo Brazil waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 .
Pichani muamuzi wa mchezo huo Rudi Glockner kutoka Ujerumani akisogea katika tukio hilo lillloshuhudiwa ulimwenguni kote baada ya camera zote zilizokuwa uwanjani kumulika alichokuwa akifanya Pelé.
Kutokana na tukio hilo kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma ilimlipa Pele kiasi cha dola 120,000 zaidi ya milioni 277 za kitanzania kwa kuitangaza bila kutegemea