RASMI uongozi wa Yanga umethibitisha kwamba kiungo Tonombe Mukoko hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22 kwenye mechi ambazo zimebaki.
Kiungo huyo anakwenda kujiunga na kikosi cha TP Mazembe kwa ajili ya kuendelea kufanya kazi ya mpira ambayo ameichagua.
Sababu kubwa ya kiungo huyo kuondoka ni makubaliano ya pande zote mbili kati ya TP Mazembe na Yanga.
Yanga wamemchukua Chico Ushindi ambaye ni kiungo na TP Mazembe wao wamemchukua kiungo Mukoko.
Mchezo wa mwisho wa Mukoko kucheza akiwa na jezi za Yanga ilikuwa mbele ya Mbuni FC ambao ulikuwa ni wa kirafiki ulichezwa Uwanja wa Sheik Amri Abeid na Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.
Mabao yote yalikuwa ni mapigo ya penalti na aliyefunga alikuwa ni Mukoko pia Chico aliweza kucheza kwenye mchezo huo na alisababisha penalti moja ilikuwa ni Januari 19,2022.
Yanga wamesema:”Tunashukuru sana kwa mchango wako nahodha msaidizi wa klabu yetu ya Yanga. Tunakutakia kila la kheri na mafanikio kwenye klabu yako mpya ya TP Mazembe,”.