Hospitali Yatakiwa Kumlipa Mgonjwa Milioni 40 Baada ya Kumpa Majibu ya Uongo ya Vipimo Kuwa ana Cancer


Kituo kimoja cha kutolea huduma za matibabu kilichopo Mombasa Kenya kimetakiwa na Mahakama kulipa fidia ya Ksh. milioni 2 (Tsh. milioni 40) kwa Mgonjwa aitwaye Roberto Macri baada ya kumpa majibu ya uongo ya vipimo kuwa ana cancer wakati hana cancer.

Jaji wa Mahakama ya Malindi, Julie Oseku amesema Mgonjwa huyo alifika Kituoni hapo 'Jamu Imaging Centre' akiwa na changamoto ya kupata shida ya kumeza chakula na akaambiwa ana 'Cancer Stage Four' hali iliyomlazimu kusafiri hadi Italia ambako aliambiwa hana Cancer.

"Mgonjwa kama asingeambiwa ana Cancer asingelazimika kutumia gharama kwenda Italia baada ya kuwa na hofu, pia majibu yalimsababishia stress na maumivu zaidi ndio maana aliporudi tu kutoka Italia akafungua kesi" ——— Mahakama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad