Kutana na mwanamama aitwaye Valeria Levitin (39) tokea nchini Hispania ambaye inaaminika kuwa ndiye mwanadamu mwembamba kuliko wote ulimwenguni
Valeria ambae ameingia katika kitabu Cha Rekodi za Dunia ,anaeonekana Kama 'skeleton' na ana Uzito wa Kilogram 27 tu, huku asilimia kubwa ya mwili wake ukiwa ni mifupa.
Sababu iliyopelekea Valerie kufikia rekodi hii, ni tabia yake ya kutopenda kula kabisa toka akiwa na umri miaka 19. Kitaalamu tabia hii inaitwa 'Anorexia' , ambapo inaanza taratibu Kwa mtu kupenda diet iliyopitiliza na kujikuta hana mapenzi na Chakula kabisa.