Jamaa Ajisalimisha Polisi Baada ya Mzigo Alioiba Kukwama Mabegani



 
Jamaa mmoja jijini Dar es Salaam, Tanzania amejikuta pabaya baada ya mzigo wa mahindi aliokuwa ameiba kumkwama mabegani.

Frank Japhet, 23, mkazi wa Mbezi, jijini Dar es Salaam, amelazimika kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani, baada ya mzigo huo kukataa kutoka mabegani.

Jamaa ajisalimisha polisi baada ya mzigo alioiba kukwama mabegani (Picha/Video)
Japhet mkazi wa Mbezi, jijini Dar es Salaam, amejisalimisha Polisi baada ya mzigo alioiba kukwama mabegani. Picha: Blobal Publishers
Wakati akihojiwa kituoni hapo, mtuhumiwa amesema mzigo huo, uliokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 20, uliofungwa kwenye gunia aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani mwendo wa 7PM usiku wa kuamkia Alhamisi, Mei 3, 2018.


Mshukiwa huyo ameongezea kuwa, aliondoka na mzigo huo hadi eneo la kituo cha basi cha Mlandizi alinuia kuuacha kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, na hapo ndipo mzigo huo ulikataa kutoka mabegani.


 
Kirinyaga: Mwanamke Aua Mchumba Wake na Kutupa Mwili Wake Mtoni
Je, Rick Ross alilala kitanda kimoja na Mwalimu Rachael wakati wa 'concert' yake Nairobi?

Jamaa ajisalimisha polisi baada ya mzigo alioiba kukwama mabegani (Picha/Video)
Japhet amedai kuwa, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke lakini ulikataa kutoka. Picha: Global Publishers
Japhet amedai kuwa, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao na alipohisi kuchoka ndipo akaamua kujisalimisha polisi.

Kulingana na ripoti ya mtandao wa Global Publishers ambayo TUKO.co.ke imeisoma, Japhet hadi wakiandika taarifa kuhusu tukio hilo, alikuwa bado ameubeba mzigo huo huku polisi wakisubiri mwenye mali auchukue.


Binti avaa 'nusu uchi' akiuza maji barabarani, watu wazua mjadala mitandaoni

Jamaa ajisalimisha polisi baada ya mzigo alioiba kukwama mabegani (Picha/Video)
Mshukiwa aliuiba mzigo huo kwa mama mmoja mwendo wa 7pm usiku wa kuamkia leo. Picha: Global Publishers
Polisi wamesema tayari wametuma taarifa kwa yeyote mwenye mzigo huo kufika kituoni hapo ili kuuchukua na kumnusuru Japheth.

Mtandao huo baadaye ulimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwanai, Kamishena Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna Warioba naye akasema:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad