Je Unaona Azam ya sasa Chini ya Moallin inavyogonga Pira Pizza?


Simu Moja kwako @abdulkarim.amin Popat

Nimeandika meseji nmefuta, nikaandika tena nikafuta. Mimi [ @kapteiny_eric ] nmeona nikupigie simu moja tuzungumze na nikuulize maswali machache.

Abdulkarim Popat nadhani Unakumbuka Azam walivyokua wanacheza chini ya Artistica Cioaba ? — Jibu baki nalo.

Unakumbuka pia Azam walivyokua wanacheza Msimu mzima chini ya George Lwandamina ? — Jibu baki nalo.

@abdulkarim.amin , Je unaiona Azam ya sasa inavyocheza chini ya Kocha, Abdihamid Moallin (The African Pep Guardiola) ambae hana hata miezi mitatu tangu achukue timu??

Je AbdulKarim Popat, unaona Jinsi ambavyo Kocha la Mpira linavyoamini vijana wenye talent? Tepsi Evance ameanza kung’aa chini ya Moallin, Paul Peter karudishwa Azam chini ya Moallin, Kenneth muguna anacheza kama Sergio Busquet chini ya Moallin, Kipa Ahmed Salula anadaka kama nyani

Je unaona Azam ya sasa chini ya Moallin inavyogonga Pira Pizza? Kama Kusoma hujui ata Picha hauoni Sheikh?

Kama wewe umeshindwa kuona, Sisi wapenzi wa mpira tunakuonyesha kwa herufi kubwa ABDIHAMID MOALLIN ni KOCHA LA MPIRA.

Huyu ni Kocha ambae kaibadilisha Azam kiuchezaji ndani ya muda mfupi sana, Azam inapata matokeo ‘Comfortably’.

Na hata Azam isipopata matokeo, bado utaridhika na Soka maridhawa linalochezwa hapo kati.

Mm sio wakala, Mm sio Mkurugenzi wa Ufundi, ila kama nmeweza kuona Moallin ni Kocha mzuri, basi mtie mkataba wa Miaka minne, mpe wachezaji wa maana, KOCHA LA MPIRA lifanye kazi bila presha, UTANISHUKURU BAADAE!

AbdulKarim Popat Usiitupe Dhahabu Mchangani! Jumapili njema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad