Jeshi la Guinea Laamuru Timu ya Taifa Kurejesha PESA za Marupurupu Walizokuwa Wamepewa Endapo Wangetwaa Ubingwa wa AFCON 2021.


Serikali ya taifa la Afrika la Magharibi la Guinea imewataka wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa kandanda waliokuwa huko nchini Cameroon kurejesha pesa za marupurupu walizokuwa wamepewa endapo wangetwaa ubingwa wa AFCON 2021.

Hatua hiyo ya serikali ya Guinea inayo ongozwa na Kanali Mamady Doumbouya imekuja baada ya Wachezaji hao kutakiwa kulitwaa kombe la fainali za mataifa ya Afrika na mwishowe kushindwa kufanya hivyo.

Endapo wangefika hatua ya ¼ fainali, kila mchezaji wa timu ya taifa ya Guinea angelipwa shilingi milioni 23.
Wangefika hatua ya ½ fainali, kila mchezaji angelipwa shilingi milioni 28 na nusu.

Na wangefika hatua ya fainali na kutwaa taji, kila mchezaji angelipwa kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 69.
Pesa zote hizo zikizidishwa kwa idadi ya wachezaji 30 wa kikosi hicho, kikosi cha timu ya taifa ya Guinea kinatakiwa kurejesha zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni 3. 66 za posho na marupurupu.

DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA BURE KUPATA HABARI KAMA HIZI WA KWANZA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad