Jeshi la Polisi limetolea ufafanuzi kile ilichokiita upotoshaji kuhusiana na tukio la kujinyonga hadi kufa kwa Askari Grayson Mahembe Mkoani Mtwara ambapo limeendelea kusisitiza kuwa alijinyonga akiwa katika Mahabusu ya peke yake ambayo aliwekwa kufuatia tuhuma za mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini.
"Kuhusu mazishi yake, Askari anayefariki kwa kujitoa uhai hazikwi kijeshi, hakuna gwaride la mazishi na risasi au mabomu ya kishindo kwani anahesabiwa kuwa hajafa kishujaa na hastahili heshima hiyo"