“Wiki ya mwisho ya kuingia mwaka mpya nilipata homa, niliugua sana, nadhani mnaona hata sauti yangu haijakaa sawa. Sikuwa katika nafasi ya kuweza sema chochote, hali ilikuwa ngumu.
“Kuna watu walikatakata mambo, wakatengeneza clip na kusababisha mjadala ambao umesabaisha usumbufu. Nimeona tukutane niweke sawa hili suala.
“Hakukuwa na lolote la kukashifu wala kudharau juhudi za serikali, na katika mazungumzo yetu, niliwasisitiza kulipa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa kufanya hivyo tunaisaidia serikali katika kujitegemea,” - Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari ofisi za Bunge, Dodoma, leo Jumatatu.