Job Ndugai "Nimeumia Sana Kuonekana Napinga Mkopo"

 


"Katika jambo lililoniuma ni kwamba ni kuonekana napinga mkopo wa Shilingi trilioni 1.3, mfano jimbo langu Kongwa tumepata madarasa 112 kupitia fedha hizo, na hatujawahi kupata madarasa mazuri kama madarasa yaliyojengwa kipindi hili.


"Kwa mara ya kwanza watoto wetu wanakwenda kusomea madarasa ambayo yana vigae, ya kisasa. Na hili lisingetokea kama siyo uthubutu wa Rais Samia Suluhu kwenda alipoenda na kufanikiwa kupata fedha kiasi cha Shilingi trilioni 1.3.


"Sisi Bunge ni sehemu ya hizi fedha Shilingi Trilioni 1.3, itakuwa ni dhambi kubwa kuwavunja nguvu viongozi wetu. Tumtie moyo Rais wetu, Tumtie nguvu,” - Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari ofisi za Bunge, Dodoma, leo Jumatatu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad