JOHARI kutoka Bongo Muvi anasema kuigiza Ndoa huku umevaa na Shela wakati sio Ndoa ya kweli Ndo kunawafanya wasanii wengi wa Bongo Muvi wasiolewe.
Pia anasema Amejifunza kuigiza Ndoa ni kujipa NUKSI kwenye maisha Halisia Maana kwenye ulimwengu wa Roho unakuwa ushaolewa.
“Mashela ndiyo yameharibu kila kitu na hata ndoto za kuolewa kweli kwa sababu inaonekana kiroho tumeshaolewa, sasa kama mimi jamani nimevaa mashela mara tatu hiyo unaichukuliaje sasa kuna ndoa tena hapo? Kwa hiyo nimeseme tu kwamba mashela yameondoka na ndoa zetu,” anasema Johari ambaye amekuwa akitamani kuolewa kwa muda mrefu."
Je Unakubaliana na Anachokiamini Muigizaji huyu Mkongwe?.