Takriban watu sita wameuawa na vijiji kuchomwa moto na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab katika mji wa pwani wa Lamu nchini Kenya, katika tukio lililotokea leo Jumatatu Januari 3, 2021.
Jeshi la polisi nchini humo linaeleza kuwa wapiganaji waliokuwa na silaha nzito walishambulia vijiji vya eneo la Widho na kusababisha maafa makubwa.
Kundi hilo la wanamgambo limefanya mashambulizi mengi katika kaunti ya Lamu ambayo iko mpakani mwa Somalia katika maeneo yanayofikiriwa kuwa ngome ya kundi hilo linaloshirikiana na mtandao wa Al Qaeda