Kesi ya Mbowe na wenzake yaanza

 


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi  leo Jumatatu Januari 10, 2022 inaendelea na usikilizwaji wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya kesi hiyo kusimama kwa siku 21 kupisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2022.

Washtakiwa tayari wameshafikishwa katika ukumbi wa Mahakama hiyo.

Tayari mawakili wa pande zote mbili nao wameshafika katika Mahakama kwa ajili yakusikiliza uamuzi hukusiana na kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Leo, Januari 10,  2022 Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo anarajia kutoa uamzi kuhusiana na kielelezo ambacho ni sare za Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania , zilizopingwa na upande wa utetezi zisipokelewe  na mahakama kutokana na kukiuka matakwa ya kisheria.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad