Khadija Kopa Akana Kutokuwa na Ugomvi na Mama Dangote "Sina Namba yake ya SIMU Ila Tukikutana Tunaongea"


Baada ya madai kuwa Diamond ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa lebo yake Wasafi ‘Zuchu’ kumeibuka tetesi kwamba urafiki baina ya Mama wa Diamond na mamake Zuchu umesambaratika.

Khadija Kopa amekuwa akizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii kwa madai ya uhusiano wa Bintiye Zuchu na Diamond Platnumz.

Tuhuma hizo ambazo hazijathibitishwa na mastaa hao, zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii. Kulingana na mitandao ya Bongo kuna tetesi kwamba Mama Dangote hakufurahishwa na habari za wawili hao kuhusishwa kimapenzi.

Khadija Kopa akizungumza kuhusu madai hayo ameeleza kwamba yeye na Mama Dangote hawaja kosana na kusema hana namba yake simu ila wakikutana uongea kama marafiki.

🗣“Sisi ni marafiki na tunaongea na kucheka, hatujawai kutofautiana. Kwa hivyo, acha kuunda vyama sisi ni watu wa kawaida ambao watoto wetu wametuleta pamoja tangu waanze kufanya kazi pamoja” alisema Khadija Kopa

Kutokana na kauli yake ya kuwa wao ni marafiki aliombwa kumpigia Mama wa Diamond simu ambapo alikataa kwa kusema hana muhimu la kumwambia.

🗣“Sijawahi kuwa na namba yake ila kama kuna kitu cha dharura , nitaipata na kumpigia. Muda mwingi nikitembelea duka la Esma namkuta yupo na tunaongea. Kujenga chuki miongoni mwetu ni kinyume cha Mungu.” alidokeza


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad