Kigogo JWTZ aeleza alivyofahamiana na Mbowe, alichohitaji



OFISA wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Denis Urio, amedai Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimueleza anatafuta kampuni za kijeshi kwa ajili ya kufunga mifumo ya mawasiliano yenye lengo la kufuatilia viongozi wa chama chake wanaotoa siri nje. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar ea Salaam … (endelea).

Pia, Urio ambaye ni mwenye cheo cha Luteni ameieleza mahakama jinsi alivyofahamiana na mwanasiasa huyo wa upinzani pamoja na washtakiwa wenzake watatu, katika kesi ya ugaidi inayowakabili.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Adam Kasekwa, Halfan Bwire na Mohame Ling’wenya ambao walikuwa makomandoo wa JWTZ, Kikosi cha 92KJ kilichopo Ngerengere, mkoani Morogoro.

Luteni Urio amedai hayo, leo Jumatano, tarehe 26 Januari 2022, mbele ya Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo, wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.


 

Luteni Urio ambaye ni shahidi wa 12 wa Jamhuri, ametoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdllah Chavula akidai alifahamiana na Mbowe mwaka 2008 baada ya mwanasiasa huyo kumtafuta kwa kumpigia simu yake ya mkononi.

Kwa mujibu wa ushahidi wa Jamhuri, Mbowe anadaiwa kumuomba Luteni Urio amtafutie makomandoo wa zamani wa JWTZ, kwa ajili ya kutekeleza njama za kufanya vitendo vya kigaidi katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kudhuru viongozi wa serikali.

Mahojiano ya Wakili Chavula na Luteni Urio yalikuwa kama ifuatavyo;


Chavula: Kuna mtu anaitwa Freeman Aikaeli Mbowe, wewe mtu huyu unafahamiana naye vipi?

Shahidi: Freeman Mbowe nimeanza kuwa na urafiki naye toka 2008 mpaka 2020.

Chavula: Unaposema umefahamiana naye mwaka 2008, unaweza ukaieleza mahakama ni katika mazingira gani yalipelekea baina ya ninyi wawili kufahamiana?

Shahidi: Nakumbuka mwaka 2008, Mbowe alinipigia simu ya mkononi akaniita kwa majina yangu


 
Chavula: Unaweza ukaieleza mahakama ilikuwa ni mwezi gani?

Shahidi: Siwezi kukumbuka mwezi wala tarehe

Chavula: Wewe ulipokea simu yake, simu yako ilikuwa na namba gani?

Shahidi: Ilikuwa na namba ya mtandao wa Voda, 0754612518


Chavula: Unaweza ukaikumbuka namba yake ilikupigia namba gani?

Shahidi: Ilikuwa ni mtandao wa Airtel hiyo namba siikumbuki

Chavula: Alikueleza nini?

Shahidi: Akanipigia simu akaniuliza wewe ndio Denis Urio askari wa JWTZ, nikamwambia ndio, nikamuulizia wewe nani, akaniambia Freeman Mbowe

Chavula: Ulikuwa unamfaham kivipi?

Shahidi: Alipojitambulisha kuwa yeye ni Mbowe sababu alikuwa anaonekana kwenye vyombo vya habari maana anafahamika si jina geni, nikamuulzia namba yangu ameipata wapi?

Chavula: Nini kiliendelea?

Shahidi: Baada ya kumpa salamau, alikwua ana-cofirm profile yangu


 
Chavula: Unamaanisha nini?

Shahidi: Anahakikisha mimi ndiye Denis Urio nikamwambia sahihi, akaniambia mimi mtu wako, kilichobaki tufahamiane kuanzia hapo tukawa tunawasiliana kwa simu uhusiano ndio ulianza

Chavula: Yeye namba yako ya simu aliitoa wapi?

Shahidi: Sifahamu alipoitoa

Chavula: Yeye alikuambia wapi ametoa?

Shahidi: Aliniambia mbona unafahamika sana, mtu akitaka namba yako ni rahisi kuipata, usiwe na wasiwasi

Chavula: Iambie mahakama kitu gani kilipelekea yeye kujua unafahamika sana?

Shahidi: Nilipotaka mimi kujua alipopata mawasiliano yangu, mimi akaniambia mbona watu wananifahamu

Chavula: Hayo maneno wakati gani alikutamkia?

Shahidi: Wakati huo mara ya kwanza kuwasiliana na mimi

Chavula: Mliwasiliana kwa njia gani mara ya kwanza?

Shahidi: Kwa njia ya simu ya mkononi, mawasiliiano yetu yaliendelea, tuliendelea kuwasiliana alikuwa akinipigia simu, akinitumia ujumbe.

Chavula: Katika mahusiano yenu ni wakati gani mlikuja kukutana ana kwa ana?

Shahidi: Mahusiano yaliendelea mpaka 2012, ambapo niliona naye ana kwa ana

Chavula: Mlipokutana ilikuwa tarehe ngapi?

Shahidi: Siwezi kukumbuka tarehe wala mwezi

Chavula: Mlipokutana na Mbowe ni mazingira yepi yalipelekea ninyi kukutana 2012?

Shahidi: 2012 nilikuwa maeneo ya Mibulani, Dar es Salaam nimepokea simu kutoka kwa Mbowe, kama alivyokuwa kawaida yake ananipigia tukawasiliana akaniambia uko wapi, nikamwambia niko maeneo ya Mibulani. Akaniambia kuna kitu cha muhimu nataka tuongee tunaweza kuonana

Chavula: Ulimwabia nini?

Shahidi: Nikamuuliza tutaonana wapi? Akaniambia njoo Mikocheni kuna sehemu inaitwa Casa Hotel, sina uhakika na jina sababu ni muda mrefu

Chavula: Wewe ulipoambiwa hivyo ulichukua uamuzi gani?

Shahidi: Nilimwambia sijui hoteli ilipo, halafu maeneo ya Mikocheni mimi sifahamu sababu ni mgeni

Chavula: Ulifanya nini?

Shahidi: Akaniambia niende kituo cha tax nimwabie dereva wa tax anipeleke Casa Hotel

Chavula: Baada ya kupewa maelekezo maamuzi yako yalikuwa yepi?

Shahidi: Nilitafuta dereva tax anayejua ilipo nikampata, basi nikaanza safari ya kwenda Casa Hotel.

Nilivyofika nikampigia simu akapokea, akanielekeza pale Casa Hotel kuna kiti kimepangwa kuna meza, kuna watu wanne wamekaa mbalimbali, akaniambia shuka kwenye gari njoo sehemu yenye baa.

Baada ya kufika akaniambia huyo anadai shilingi ngapi ya nauli, nikamwambia Sh.20,000 akalipa gharama ya tax , baada ya kumpa mazungumzo yaliendelea

Chavula: Haya yote yanayokea ilikuwa majira gani?

Shahidi: Majira ya Alasiri kuanzia saa saba

Chavula: Mwingine naye aliyekuwapo?

Shahidi: Hapakuwa na mtu mwingine tofauti, yaani mimi na yeye

Chavula: Ileze mahakama nini mlichozungumza wakati ule?

Shahidi: Baada ya kukutana alinieleza mambo makubwa matatu, la kwanza alikuwa anataka kujua profile yangu mimi, nina jina, elimu gani, ninafanya kazi gani na cheo gani, ndiyo alikuwa ananidodosa

Chavula: Wewe ulimjibu nini?

Shahidi: Nilijibu kadiri alivyoniuliza swali lake, majibu niliyompa nilimwambia sina rank (cheo).

Akaniuliza Mimi nyumbani ni wapi, nikamwabia Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Mjini

Chavula: Jambo gani lingine mlilozungumza?

Shahidi: Hoja ya pili alitaka kujua msimamo wangu dhidi ya vyama vya upinzani

Chavula: Majibu yako yalikuwa yepi?

Shahidi: Nilimjibu taratibu za kazi yangu siruhusiwi kufungamana na chama chochote, ila kwa viongozi walioko madarakani.

Chavula: Lipi lingine mlilozungumza?

Shahidi: Hoja ya mwisho aliniuliza anahitaji makampuni ya kijeshi kufunga mifumo ya mawasiliano kwenye ofisi zao, kama iliyoko jeshini, jeshini wanafunga mifumo ya mawasiliano

Nikamuuliza swali kwa nini anataka makampuni ya Jeshi akasema kwa sababu ya kufuatilia viongozi wenzao wanaotoa siri nje ya chama

Chavula: Wewe majibu yako yalikuwa yapi?

Shahidi: Nilimshauri aende kwenye taasisi atapata, baada ya hapo tuliachana, akaagiza tax ikaja pale, akalipa hela sijui alilipa kaisi gani.

Luteni Urio anaendelea kutoa ushahidi wake
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad