Kijana Atuhumiwa Kumuua Mpezi Wake



Maafisa upelelezi nchini Kenya wamemkamata kijana aitwaye Brian Waweru mwenye umri wa miaka 25, kwa tuhuma za utekelezaji wa mauaji ya kinyama aliyoyafanya kwa mpenzi wake Everlyn Wanjiru (24), katika eneo la Ndenderu, Kaunti ya Kiambu.

 

Brian na Wanjiru kwa pamoja walikuwa wakimiliki saloon ya kiume huko Thindigua na wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu kabla ya kuanza kutofautiana baina yao, mwezi Oktoba, mwaka jana.

 

Wakati anatekeleza mauaji hayo, Waweru alikuwa na kesi ya kumshambulia mchumba wake huyo katika Mahakama ya Kiambu na alikuwa nje kwa dhamana.

 

Baba wa Wanjiru ameeleza kuwa mtuhumiwa pamoja na familia yake, walimfuata mzee huyo na kumuoma wayamalize kifamilia badala ya mahakamani jambo ambalo familia zote mbili ziliridhia, lakini mahakama ilikataa, wawili hao kurejea tena kwenye mahaba yao tangu wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka (Desemba) kabla ya mauaji hayo kutokea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad