Kijana mwenye umri wa miaka 19 aitwae Jack Sweeney amekataa ofa ya $ 5000 ( Tsh. Milioni 11.5 ) kutoka kwa Tajiri namba 1 Duniani Elon Musk ambaye yupo tayari kumlipa ili aifute akaunti feki ya twitter inayotweet safari za Ndege binafsi ya Bilionea kila inapopaa.
Akaunti hiyo ambayo Jack ameipa jina la Elon Jet ina followers zaidi ya 150,000 na huwa ina-tweet kila Private Jet hiyo inapopaa na kutua pamoja na muda ambao inatumia iwapo angani.
Meseji ambazo zimesambaa mtandaoni zinaonesha Elon akiwa amemtumia Kijana huyo akimuomba aifute akaunti hiyo kwasababu ina hatarisha usalama wa Elon na akamuahidi pia kumpa fedha ambazo zitamsaidia kwenye masomo na vitu vingine.
Kijana huyo amekataa ofa ya Elon na kusema fedha hiyo ni ndogo ukilinganisha na furaha anayoipata kwakuwa moyo wake unapata raha kwa kufanya anachokitaka na kusema raha hiyo haiwezi kununuliwa kwa fedha, hata hivyo Kijana huyo amemshauri Elon kutafuta program itakayomsaidia kublock Ndege yake isiwe inafuatiliwa.
"Inaonesha Elon ameufanyia kazi ushauri wangu na anatumia hizo program napata shida kum-track lakini bado hawajaweza kunizuia” ——— Sweeney.