Kijembe cha Maua Sama kwa Nandy Na Zuchu

 


BAADA ya msanii Maua Sama kuposti kunako Mtandao wa Twitter kwa kuandika; “Kwani ikitokea hujaimba Amapiano unaweza kufutiwa cheti cha usajili Basata? Au utapokonywa Nida na passport? Nipo zangu sehemu hapa nakunywa soda nasikiliza Zai, Utu na I Wish (on repeat), nipo airport njooni mnipige…” basi ndipo mambo yakaibuka.

Kwa mujibu wa wadadavuzi wa mambo, maelezo ya Maua Sama ni kijembe hivi kwa Nandy na Zuchu kwa sababu ndiyo wasanii wa kike ambao wako kwenye levo moja na wao wawili wametoa ngoma za Amapiano ila yeye tu ndiye bado na hategemei kuachia Amapiano.

Hii vita ya Amapiano na Bongo Fleva ni kubwa mno kwa sababu kila msanii anafanya anachoona ni sahihi kwake, muziki hauna mipaka, hata mtu akitoboa kwa Amapiano ni sawa tu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad