Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo wakiwa wanaangalia namna soko la Karume lilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 16, 2022.
Dar es Salaam. Msemaji wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Masoud Isa licha ya kulipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kufanya kazi nzuri ya kudhibiti moto uliounguza soko la Karume lakini ameimeomba Serikali kuwatengenezea wafanyabishara miundombinu mizuri itakayowasaidia kukabiliana na ajali kama hizo zisilete madhara makubwa.
Amesema ajali ya moto kutokea kwenye soko hilo la Karume (Mchikichini) ni mara ya tatu na muda wote huo wafanyabishara wamekuwa wakipata hasara kubwa ya mali zao kuteketea kwa moto.
Akizungumza Leo Januari 16, 2022 kwenye soko hilo, Kiongozi huyo ameomba Serikali watengeneze miundombinu wezeshi ikiwemo masinki ya kudumu yasiwe ya kuungua moto huku akimuomba Ras Samia Suluhu Hassan kusimamia.
"Kutokea majanga kama haya kwenye soko hili sio mara ya kwanza ni mara ya tatu sasa na kipindi chote watu wanapoteza mali zao tunaiomba serikali itutengenezee miundombinu mizuri ya kukabiliana na hili tatizo ikiwemo kujengewa masinki ya kudumu,"amesema Isa
"Kutokea majanga kama haya kwenye soko hili sio mara ya kwanza ni mara ya tatu sasa na kipindi chote watu wanapoteza mali zao tunaiomba Serikali itutengenezee miundombinu mizuri ya kukabiliana na hili tatizo ikiwemo kujengewa masinki ya kudumu,"amesema Isa
Kiongozi huyo amewaomba wamachinga wenzake kuendelea kuwawatulivu wakati serikali inaunda Kamati ya kuchunguza ili kubaini kiini cha tukio hilo.
Naye Afisa Masoko wa Jiji la Ilala, Victoria Rugemalira amesema soko hilo lilikuwa na wafanyabishara zaidi ya 3500 waliokuwa wamesajiliwa Kwenye taarifa zao.
"Tulikuwa na watu wa mitumba 2330,wa nguo za kawaida viatu pamoja na vyombo 589 wakati wenye kanga na vitenge 440 na wenye vioski 175 hao walikuwa Kwenye data bezi yetu lakini kunawengine walikuwa wanaongezeka ikiwemo walemavu ambao tulikuwa tunaendelea kuwasajili,"amesema
Amesema walisema awali walikuwa na mpango wa muda mrefu wa kuboresha soko hilo ili liwe na miundombinu ya kisasa kwa kujenga jengo la ghorofa tatu lakini kwa bahati mbaya ajali imetokea.
"Pamoja na hivyo bado mpango wa kuboresha bado uko palepale isipokuwa tunawaomba wafanyabishara wawe na subira,"amesema