MASTAA wa zamani wa kimataifa nchini, wamemkingia kifua nahodha wa Simba, John Bocco kuwa kushindwa kwake kuanza kwa kishindo Ligi Kuu Bara msimu huu inatokana na mwili wake kuwa na fatiki.
Msimu ulioisha Bocco alikuwa mfungaji bora akifungua mabao 16, chini ya kocha Didier Gomes, lakini msimu huu chini ya Pablo Franco licha ya kuanzishwa hajafunga bao, huku Meddie Kagere aliyemaliza msimu uliopita na mabao 13, amefunga manne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti , nyota wa zamani wa Simba na Yanga, walisema Bocco akipata mapumziko mazuri ya kuurejesha mwili wake atapiga kazi kwa kasi.
Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ anayeshikilia rekodi ya kufunga jumla ya mabao 153 kwa misimu 13 alisema, “Bocco ni straika mwenye rekodi yake kwa wazawa ya mabao 139 kwa misimu aliyocheza, siamini kama kutoanza kwa kufunga atakuwa ameishiwa kiwango, binafsi naona ametumika sana mwili wake utakuwa una fatiki,” alisema Chinga One, huku Ally Pazi Samatta, baba wa Mbwana Samatta alisema, “Nipo tofauti kidogo na mtazamo wa wengine wanaona Simba ina wachezaji wabaya, kilichopo sio Bocco peke yake, wachezaji wengi wana fatiki, huyo Kagere hakuwa na nafasi kubwa msimu ulioisha ndio maana anacheza,” alisema.
Alishauri wachezaji ambao hawakuwa na nafasi msimu ulioisha, wapimwe kupitia Kombe la Mapinduzi ili kuwapa muda wa kupumzika wale ambao walikuwa panga pangua kikosi cha kwanza. Naye beki wa zamani wa timu hiyo, Boniface Pawasa alisema anachokiona kwa Bocco na wachezaji wengine wanasumbuliwa na fatiki, huku akiwataka mashabiki watulize presha dhidi yao