“Kwanza mimi Julio huwa ninasema kwa waandishi, mimi ninapenda sifa kuliko hela. Namungo ingekuwa timu mbovu hata nisingetia mguu kisa tu nipate hela.
“Nipate hela kisha nifedheheshe jina langu, hilo siwezi fanya, hivyo mpaka uone nimechukua maamuzi ya kuja hapa ni kwa kuwa Namungo wana timu nzuri.
“Yule mwalimu kutoka Zambia ambaye nitashirikiana naye hapa ni mwalimu hasa, kwanza ana leseni A, pia ni mkufunzi, tuna mwalimu mmoja mzito, na mimi Julio ni mzito, kisha nikaingie kwenye timu ya hovyo, hilo jambo siyo sawa.
“Morocco amefanya kazi kubwa, sisi tutaangalia mapungufu kisha tuyafanyie kazi,” Jamhuri Kihwelo Julio kuhusu kukubali kuitumikia @namungofc ambapo amekuwa Kocha Msaidizi.
Ameyasema hayo akiwa Zanzibar ambapo timu yake inashiriki katika Kombe la Mapinduzi.