↪️Kwanza kabisa ni kweli Simon Msuva yupo nchini Tanzania na hajarejea nchini Morocco ambapo timu imeshaanza mazoezi tangu January 5, huko Agadir, Morocco
↪️Waandishi kadhaa kutoka nchini Morocco na vyanzo vyangu kutoka Casablanca vinadai kuwa Kuna shida ya kimaslahi kati ya Msuva na Wydad
↪️Timu nyingi za Kiarabu Kuna utata kuhusu signing fee, Inasemekana Msuva licha ya kulipwa mshahara na marupurupu ila changamoto ni kuwa hawajamaliza signing fee yake
↪️ Kutokana na mvutano huo Msuva amegomea kurejea nchini Morocco mpaka pale jambo lao litakapokuwa sawa bin sawia Kabisa
↪️Swali la kwanza kwa chanzo changu, je Msuva anaweza kuachana na Wydad na akarejea Tanzania? Jibu ni kuwa Hilo linawezekana ila kwa njia tatu kubwa
↪️Ya kwanza ni Msuva kusaini timu yoyote Tanzania huku sakata lake likiendelea, hii ni kama Chama alivyosaini Simba akitokea Dynamos au Kichuya na ile klabu ya Misri, unaicheza karata ya hatari
↪️Ya pili ni Msuva kukaa chini sasa na Wydad kisha kuvunja rasmi mkataba kwa makubaliano (mutual agreement) kama Chama na Berkane kisha akarejea nchini kucheza
↪️ Ya tatu, ni Msuva kwenda FIFA kudai haki yake, ijapo hii njia ni ngumu na huchukua muda, kama ilivyomtokea Shabaan Chilunda ikamlazimu akae nusu msimu bila kucheza na hawaoni Msuva akipita njia jii
↪️Nikauliza Msuva ikitokea anasaini anaenda Simba au Yanga? Jibu ni kuwa wao wanatazama maslahi zaidi, klabu yoyote yenye maslahi mazuri itapewa nafasi, ila mpaka sasa focus ya Msuva ni kupata pesa yake na kurejea kucheza Wydad au sivyo arejee nchini
Msuva sio kama anashinikiza kuondoka Morocco bali anashinikiza malipo yake anayodai
Lolote linaweza kutokea kwa muda wowote kuanzia sasa, what a busy January
That's it for now
By jr_farhanjr