No title



KURA aliyopiga Mtanzania Mbwana Samatta kwa straika Robert Lewandowski wa Bayern Munich, imemfanya nyota
huyo aibuke mshindi waTuzo za Mchezaji Bora wa FIFA, huku akiwatosa kabisa mastaa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.


Samatta anayekipiga Klabu ya Royal Antwerp ya Ubelgiji na nahodha wa Taifa Stars, alikuwa mmoja kati ya wadau waliopiga kura hiyo ambapo tuzo hizo zilifanyika juzi usiku katika Jiji la Zurich, Uswisi yalipo Makao Makuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).


Katika kura zake tatu alizopiga kama nahodha wa Tanzania, ya kwanza Samatta ilikuwa kwa Mpolandi, Lewandowski, ya pili alimpigia mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah pia ni nahodha wa Misri na
ya tatu ilienda kwa kiungo Muitaliano anayekipiga Chelsea, Jorginho.


Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen yeye kura yake kwanza ambayo kwa mujibu wa FIFA inakuwa na pointi tano, alipiga kwenda kwa Salah, ya pili kwa Lewandowski na ya tatu kwa Messi.


 
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers ambao ni wachapishaji wa gazeti hili na Spoti Xtra, Saleh Ally akiwa ndiye mwandishi pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa na FIFA kupiga kura hizo, yeye karata ya kwanza ilitua kwa Salah, kisha Jorginho kabla ya kumaliza na Lewandowski.

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad