Tahasisi ya Basata imeamua kurudisha tuzo za wanamziki ambazo kipindi fulani zilishindwa kufanyika kutokana na sababu mbalimbali.Ukiwa mdau mkubwa wa mziki wa Tz unaishauri Basata nini wafanye ili tuzo hizi ziwe Bora na ziwe na muendelezo mzuri?
Nimeona Basata wameita baadhi ya wasanii wakubwa kwenye mualiko walitoa kabla hawajafanya uzinduzi kama Diamond Platnumz, Alikiba na Harmonize pekee na kwa upande wa wasanii wa kike wameitwa Nandy na Zuchu pekee
Swali langu kwa kufanya hivi mbona wameonesha ubaguzi wa waziwazi kwanini wachague baadhi ya wasanii wakubwa wakati tuzo ni za wasanii wote hao Diamond,kiba harmonize, Zuchu na Nandy vigezo gani vimetumika kuwaita hawa pekee? Unadhani hawa ndio watawakilisha Maoni ya wasanii wote?
Kwanini Basata wasikae na wasanii wote badala ya kuwachagua wachache Tena wale wakubwa pekee?