Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Taarifa kutoka kwa familia hiyo zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji.
Akizungumza leo ljumaa Januari 28, 2022 na Mwananchi, Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa matatizo ya tumbo.