"Ninaandika haya kwasababu nimeguswa na pia mimi ni mmoja wa wahanga wa TUKIO/MATUKIO ya aina hii….Kwahiyo naelewa unavyojisikia wakati huu.
Wema,
Kilichotokea kimetokea…Uombwe msamaha,usiombwe msamaha HAKUNA KINACHOWEZA KUFUTA/KUBADILISHA (JAPO NIMEFARIJIKA KUONA MUHUSIKA AMECHAGUA HEKIMA YA KUFANYA HIVYO)
Kitu pekee kinachoweza kubadilisha haya yote ni WEWE MWENYEWE.
Kuna mambo mawili tu yamekuwa yakinisaidia binafsi na kama utaona yanafaa utajaribu pia..!
1.Samehe hata kama hujaombwa msamaha (Hii ni kwa faida yako na sio ya unayempa msamaha)
2.Ilinde NAFSI yako Kuliko Kitu chochote.
Najua kuna muda ni ngumu…tumeumbwa kwa Nyama na damu…Kuna Muda havivumiliki and its okay ku react ila hakikisha reaction yako haizidi kuumiza/kubomoa NAFSI yako..!
Binafsi naamuaga kuwa jasiri kwenye mengi lakini haimaanishi hayaumizi…ila kwasababu ninajua kuumia kwa kupitiliza kutazidi kuibomoa NAFSI yangu…huwa nachagua kuumia kidogo na kutafuta njia sahihi ya ku deal na kinachoniumiza.
Mwisho…Kwa mliochagua kutumia muda wa maisha yenu kuwafanya wengine waumie…wawe wanyonge….wajisikie vibaya nk NIWAKUMBUSHE tu Hii ni DUNIA na ina mzunguko mkubwa sana….Sio kila kitu anachopitia mtu AMEKIOMBA au ANAKIFURAHIA….vingine Ndo njia pekee MUNGU anayotumia kutoa FUNZO kwa KIUMBE chake…Na hujui kesho kwako,kwa ndugu au hata jamaa yako MUNGU atatumia njia ipi…..TUWE NA KIASI…TUWE NA AKIBA ya MANENO na MATENDO yetu pia.
With Love,
Mama G❤️"