MADAKTARI 11 wamemwandikia barua ya wazir Rais wa Ghana, Nana Addo Dankwa Akufo-Addo kutoa mwongozo ikiwezekana kusitisha usambazaji wa chanjo za corona kwa ajili ya kupambana na janga la corona kwa taifa hilo.
Umoja wa Madaktari hao wamesema kuwa kutokana na tafiti zilizofanywa, inaonyesha madhara ni mengi zaidi kuliko faida za chanjo hiypo.
Katika waraka wao walioutoa juzi Jumatatu, Januari 10, 2022, madaktari hao ambao wanajiita Madaktari wa Ghana Wenye Wasiwasi wameeleza namna ambavyo Uingereza na Israel bado wanabishana kuhusu usalama wa chanjo hizo na wingi wa wagonjwa na vifo licha ya mamilioni ya watu kuchanja katika nchi hizo.
“Hizi nchi zina watu wengi waliochanja, lakini bado wanatengeneza na kusambaza chanjo ya ku-boost (kuchopchea chanjo), na sasa wanahangaika na huyu kirusi mpya wa Omicron namna ya kumdhibiti.
“Fikiria nchini nzima tumechanja takribani asilimia 50 ya wananchi wote, tutaendelea na hizi chanjo za booster kwa miezi mitatu hadi minne kuendelea kudumisha chanjo hii kwenye mwili?
“Wapi utakuwa mwisho wa hii chanjo, lini itakuwa mwisho wa gonjwa hili kusambaa, nchi yetu inao uwezo wa kifedha wa kumudu kama taifa?
Madaktari hao wametoa mtazamo wao kuwa kwa Serikali kuagiza chanjo hiyo iwe lazima kwa kila mwananchi ni biashara na faida kwa makampuni makubwa ya madawa duniani.
Aidha, madaktari hao wamesema kuwa Ghana na Afrika kwa ujumla wamefanya vyema katika kudhibioti janga la corona tofauti na mataifa ya Ulaya kabla hata ya ujio wa chanjo hizo lakini wanashangaa mataifa ya Afrika kulazimishwa kuchanja.
Madaktari hao ni Dr Timothy Oblijah Armah, Dr Bismark Opoku-Asare, Dr Faisal Adjei, Dr William Ghunney na Dr Bernard Boateng Adjei. Wengine ni Dr Doreen Oye Agyei, Dr Michael Agyemang-Wiredu, Dr Richard Fayah, Dr Sedem Cyril Klinogoh, Dr Phil Dowuona na Dr Emmanuel Awuttey.