Mafao ya Ndugai balaa, kuvuna mamilioni



ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ambaye alilazimika kujiuzulu wiki iliyopita, atavuna mamilioni ya shilingi kila mwezi, kama malipo yake ya kustaafu, ikiwamo asilimia 80 ya mshahara wa Spika atakayekuja kurithi nafasi yake hadi kifo. Anaripoti Gabriel Mushi…(endelea).

Taarifa kutoka bungeni Dodoma na serikalini zinasema, pamoja na kujiuzulu wadhifa wake, Ndugai atalipwa asilimia 50 ya mafao ya fedha alizopata akiwa Spika.

Kwa mujibu wa Sheria ya viongozi wastaafu wa kisiasa ya mwaka 1999, inayozungumzia mafao ya Spika, inaeleza kuwa kiongozi anayeacha nafasi ya Spika wa Bunge, atakuwa na haki ya kupata mafao yafuatayo, baada ya kuacha nafasi hiyo.

Kifungu cha 18 (a) kinasema, kiongozi aliyeshika nafasi ya madaraka ya Spika wa Bunge, baada ya kuacha wadhifa huo, atapewa kiinua mgongo asilimia 50 ya fedha zote, alizowahi kupokea kama mishahara wakati akiwa Spika.


 
Undani wa habari hii kujua mgawanyo wa mamilioni hayo, soma gazeti la Raia Mwema la leo Jumatatu, 10 Januari 2022.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad