Makada CCM Wajitosa Kuutaka Uspika..Sophia Simba Ndani



Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameendelea kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania.


LEO Januari 11, 2022 wamejitokeza baadhi ya wanachama kuendelea kuchukua fomu hizo katika ofisi za makao Makuu ya CCM jijini Dodoma na wengine kwenye ofisi ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.


Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu amechukua fomu hizo katika ofisi za CCM jijini Dodoma huku aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sofia Simba na akiyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye wakichukua katika ofisi ndogo za Dar es Salaam.


Baada ya kuchukua fomu hizo, Zungu amesema amefuata sheria zote za kujaza fomu ya kutaka kugombea nafasi hiyo ili wanachama wenzake wampitishe kwa mujibu wa sheria.


“Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na Chama chetu nafasi hii ina utaratibu wa kujazwa, na kuombwa kwake ni kujaza fomu ambapo viongozi wa chama watapitia maombi yangu na kutizama kama ninatosha watatoa majibu” amesema Zungu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad