Mama Dangote Aweka Rekodi "Watoto Wangu ni wa Anko Shamte"

 


MAMA mzazi wa staa wa muziki wa Tanzania, Diamond Platnumz, Mama Dangote amevunja ukimya akisema kuwa, watoto wake, pia ni watoto wa mumewe, Anko Shamte.

Inafahamika kwamba, Mama Dangote au Mama D ameolewa na Anko Shamte na hawajabahatika kupata mtoto hivyo maneno ni mengi mitandaoni hasa akishambuliwa mumewe huyo.

Ili kumaliza ubishi au kunyamazisha wazungumzaji wa ishu hiyo, Anko Shamte amemrekodi Mama Dangote akimuuliza ni jambo gani angependa liwafikie walimwengu? Je, ni uhusiano wao au ni watoto?

Katika majibu yake, Mama Dangote anasema; “Watoto wangu ni watoto wako (Anko Shamte…”

Watoto wa Mama Dangote wanaozungumziwa ambao hakuzaa na Anko Shamte ni Diamond Platnumz na Esma Platnumz.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad