IDDI Amin Dada Oumee, alikua raisi wa tatu wa Uganda, alitawala 1971 mpaka 1979, hakuwahi kuandika kitabu cha historia yake wala hakuwahi kumruhusu mwandishi yeyote kuandika habari ya maisha yake. Hii inamaanisha hakuna uhakika ni lini na ni wapi alizaliwa.
Alikotoka
Hakuna uhakika juu ya mwaka na mahali alikozaliwa. Amin mwenyewe hakuandika kumbukumbu ya maisha yake wala hakuagiza taarifa rasmi juu ya maisha yake. Vyanzo mbalimbali vinasema ya kwamba alizaliwa mnamo 1923 Koboko au Kampala. Mtafiti Fred Guweddeko amedai Amin alizaliwa 17 Mei 1928, lakini hii imepingwa. Mwanawe Amin Hussein alisema babake alizaliwa Kampala mwaka 1928. Mtoto wa Amin aitwae Hussein anasema baba yake alizaliwa Kampala mnamo mwaka 1928.
Fred Guweddeko wa Makerere University, anasema Idi Amin ni mtoto wa Andreas Nyabire alieishi kati ya 1889 na 1976. Nybire ni mmoja wa kabila la Kakwa ambalo lilibadili dini kutoka Ukatoliki kwenda Uisilamu mwaka 1910 na kubadili jina kuwa Amin Dada. Yeye mwenyewe alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa.
Kufuatana na Fred Guweddeko wa Chuo Kikuu cha Makerere Idi Amin alikuwa mwana wa Andreas Nyabire (1889–1976) wa kabila la Wakakwa, ambaye alikuwa Mkatoliki aliyehamia Uislamu mnamo 1910 akibadilisha jina lake kuwa Amin Dada na kumpa mwana wa kwanza jina hilo pia.
Iddi Amin alilelewa na mama yake bila baba kijijini katika Uganda ya Kaskazini-magharibi. Kufuatana na Gudewekko mamake Amin Assa Aatte (1904–1970) alikuwa Mlugbara aliyetibu watu na familia ya Mfalme kwa mitishamba. Amin alisoma miaka kadhaa kwenye shule ya Kiislamu huko Bombo kuanzia mwaka 1941.
Amin alijiunga na shule ya Kiislam ya Bombo mwaka 1941, aliacha shule akiwa na elimu ya darasa la nne kwa elimu ya Mwingereza na alifanya vibarua kabla ya kujiunga na jeshi la Mwingereza na kuwa ofisa wa jeshi.
Amin mwanajeshi
Baada ya miaka michache ya shule na kazi ndogondogo aliajiriwa mwaka 1946 na afisa Mwingereza wa jeshi la kikoloni King’s African Rifles (KAR) kama msaidizi wa mpishi. Baadae alidai mwenyewe kuwa alilazimishwa kuingia jeshini wakati wa vita kuu ya pili ya dunia World War II na aliwahi kupelekwa Burma.
Alihamishiwa Kenya kwa mafunzo maalumu mwaka 1947 na alikua sehemu ya kikosi cha 21 ca tattaalion Gilgil, Kenya mpaka 1949. Mwaka huo kikosi chake kilikwenda kupigania Kenya zidi ya Wasomali vita ya Shfta. Mwaka 1952 Brigadia yake ilipigana dhidi ya Mau Mau wa Kenya na alipandishwa cheo kuwa koplo mwaka 1953.
Aliingia jeshini huko Jinja akifanya kazi ya msaidizi jikoni akiendelea kupokea mafunzo ya kijeshi. Baadaye Amin alidai ya kwamba alilazimishwa kuhudumia huko Burma katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mwaka 1947 alihamishiwa Gilgil, Kenya. Mwaka 1949 alitumwa kaskazini kwa kupigania waasi Wasomalia huko. Tangu mwaka 1952 kikosi chake kilihudhuria katika juhudi za kupambana na wanamgambo wa Maumau karibu na Mlima Kenya.
Aliendela kupanda vyeo vilivyopatikana kwa Waafrika katika jeshi la KAR na muda mfupi baada ya uhuru alipewa cheo cha luteni yaani afisa kamili kama mmoja wa Wauganda wawili. Baada ya uhuru wa Uganda mwaka 1962 alikuwa kapteni halafu mwaka 1963 meja.
Mwaka 1964 alikuwa makamu wa mkuu na mwaka 1965 mkuu wa jeshi, mwaka 1970 mkuu wa mikono yote ya kijeshi. In 1970, he was promoted to commander of all the armed forces. Amin alipanda haraka ngazi kufikia cheo cha umeja wakati huo ni baada ya uhuru ikijulikana kama jeshi la Uganda, alikua kamanda kabla ya kufanya mapinduzi mwaka 1971 na kumpindua Milton Obote. Baadae alijipandisha cheo kua field marshal akiwa raisi.
Mnamo mwaka 1959, Amin alipewa cheo cha Afande Afisa Mteule (warrant officer), hiki kilikua cheo cha juu zaidi kwa askari Mweusi wa |Kiafrika katika jeshi la Mkoloni Mwingereza wakati huo. Amin alirudi Uganda mwaka huo huo, na mwaka 1961 alipewa cheo cha luteni na kuwa mmoja kati wa Waganda wawili kuwa na maafisa maalum (Commissioned Oficers).
Alipangiwa kusuluhisha mapigano ya Karamojong na kabila la Turkana la Kenya uliohusu ngo’mbe. Kufuatia uhuru wa Uganda kutoka kwa Mwingereza, Amin alipandishwa cheo kuwa kapteni na 1963 kuwa meja. Aliteuliwa kua Afisa wa pili wa majeshi ya Uganda mwaka 1970.
Mkuu wa Jeshi na mapinduzi
Amin alipandishwa cheo na waziri mkuu Milton Obote baada ya uasi wa wanajeshi katika Afrika ya Mashariki wa 1964 uliokomeshwa na askari Waingereza katika Tanganyika, Kenya na Uganda akawa makamu wa mkuu wa Jeshi aliyekuwa bado Mwingereza.
Kutoka hapa alishirikiana na Obote katika hatua za kuimarisha utawala wa waziri mkuu. Wakati bunge la Uganda lilitaka utafiti kuhusu mashtaka ya Obote kushiriki katika biashara ya siri ya pembe za ndovu kutoka Kongo Obote iliamua kubadilisha katiba na jeshi la Amini lilimfukuza Mkuu wa Dola Kabaka Mutesa kwa nguvu, halafu Obote alijitangaza kuwa rais. Sasa Amin alikuwa kanali na Mkuu wa Jeshi.
Amin alianza kuajiri hasa askari kutoka kaskazini ya Uganda mpakani mwa Sudani.
Mwaka 1970 Obote aliendelea kumpa Amin cheo cha mkuu wa mikono yote ya jeshi na ulinzi. Lakini Amin alisikia pia ya kwamba kulikuwa na mashtaka dhidi yake kutokana na matumizi ya makisio ya jeshi na mipango ya Obote kumfanyia utafiti. Hapo Amin alitumia nafasi ya safari ya Obote kwenda nje kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, akatwaa mamlaka ya serikali tarehe 25 Januari 1971.
Amin alikuwa mwanamichezo mzuri sana wa enzi zake kote katika Jeshi la Mwingereza na Jeshi la Uganda. Akiwa na urefu wa sentimeta 193 au futi 6 na inchi 4 na tambo lililo jaa, hivi vilimfanya kuwa nyota katika michezo. Alikuwa mwanamasumbwi wa uzito wa juu, muogeleaji, pia alicheza rugby kwa uwezo wa hali ya juu. Katika miaka ya 1950 alichezea Nile RFC.
Kuna usemi wa mjini kuwa alichaguliwa kama mchezaji wa ziada kaitka michezo ya Afrika Mashariki kwenye mechi dhidi ya British Lions. Amin hatahivyo hakutokea kwenye picha za mchezo huo wala jina lake halikua kwenye orodha ya wachezaji. Kutokana na maongezi na askari wenzake wa kizungu Amin alianza kujenga ushabiki na timu ya mpira ya Hayes, ushabiki huo uliendelea maisha yake yote.
Mwaka 1965, Waziri mkuu Milton Obote na Amin walishutumiwa katika mpango wa kuingiza meno ya tembo na dhahabu nchini Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mpanga huu mbao Generali Nicholas Olenga, rafiki wa aliekua kiongozo wa serikali ya Kongo Patrice Lumumba, alikuwa mmoja wa washiriki ili kusaidia majeshi ya upinzani dhidi ya serikali ya Kongo kwa siri kufanya biashara ya dhahabu na meno ya tembo kubadishana na silaha na mpangaji mkuu wa mpango huu akiwa Amin kwa Uganda. Bunge la Uganda lilidai utafiti ufanyike dhidi ya shutuma hizi.
Mwaka 1966 Obote alifuta sherehe za kiraisi zilizofanywa na Mfalme Kabaka Mutesa II wa Buganda, na kujitangaza kuwa yeye mwenyewe ni raisi na kumtangaza Amin kuwa Kiongozi wa Majeshi. Amin aliongoza mapigano dhidi ya jumba la kifalme la Kabaka na kumfanya Kabaka na familia yake kukimbilia hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza ambako aliishi mpaka mauti yanamkuta mwaka 1961.
Amin alianza kuingiza watu wa kabila lake la Kakwa na Lugbara kutoka Kusini mwa Sudani na makabila mengine kutoka Magharibi mwa eneo la Nile linalopakana na South Sudan. Watu wa Sudani ya Kusini walihamia Uganda tangia karne ya 20, walikuja kujiunga na jeshi la mkoloni. Jeshi la Amin lilijaa watu wa Sudan ya Kusini na wengi wao waliishi katika nchi zote mbili.
Milton Obote ndiye aliyekuwa rais wa pili wa Uganda ambae alipinduliwa na Idi Amin mnamo mwaka 1971. Ugomvi kati ya Obote na Amin ulianza baada ya Amin kuwa na nguvu na kubwa jeshini kutokana na kuajiri watu wa kabila lake.
Hii pia ilisaidia kusaidia majeshi ya waasi wa serikali ya Sudani ya Kusini pia jaribio la kumuua Obote mwaka 1969. Oktoba 1970 Obote alichukua madaraka makubwa jeshini na kumpunguzia Amin nguvu aliyoanza kuifurahia jeshini kwa miezi michache.
Katika miaka yake ya kushika serikali Amin alibadilika kutoka uhusiano wa kirafiki na nchi za magharibi na hasa Israeli kuhamia upande wa Muammar Gaddafi wa Libya, Mobutu Sese Seko wa Zaire, Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani ya Mashariki. Hata hivyo Amin alipata usaidizi wa ofisi ya upelelezi ya Marekani CIA iliyotuma silaha na vifaa vingine kwa jeshi lake.
Mwaka 1977 Amin alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufalme wa Maungano (Uingereza) akajitangaza kuwa alishinda na kujiongezea sifa ya CBE (“Conqueror of the British Empire”). Kuanzia wakati ule cheo chake rasmi kilikuwa “His Excellency President for Life, Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE”.
Jaribio la Amin la kutwaa sehemu za Mkoa wa Kagera wa Tanzania kwenye mwaka 1978 lilisababisha Vita ya Kagera baina ya Tanzania na Uganda na mwisho wa utawala wake. Amin alikimbia kukaa ugenini Libya na baadaye Saudia alipoishi hadi kifo chake mwaka 2003.
Mtawala wa Uganda
Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka.
Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.
Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Kanada hasa.
Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979.
Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena.
Alikufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003.
Je ni Kweli Iddi Amini Alikuwa Akila Nyama za Watu?
Hili bado ni swali ambalo halina majibu, ila watu mbali mbali wamejaribu kuliongelea hili soma hapa chini:
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amewaudhi maafisa wa serikali ya Uganda kwa kauli yake ya kudai kuwa rais wa zamani wa Uganda Idi Amin hakuwa muuaji na mla nyama za watu kama inavyosemekana. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amewaudhi maafisa wa serikali ya Uganda kwa kumtetea rais wa zamani wa Uganda Idi Amin kuwa hakuwa muuaji na mkatili kama inavyojulikana duniani.
“Tulifikiria kuwa Amin ni muuaji mla nyama za watu” Chavez alisema alipokuwa akimuongelea Idi Amin ambaye anatuhumiwa kuwaua mamia ya wapinzani wake wakati wa utawala wake nchini Uganda kwenye miaka ya 1970.
“Nina shaka kama Idi Amin alikuwa muuaji kama inavyosemekana, badala yake alikuwa mwanaharakati mtetezi wa nchi yake”, alisema Chavez.
Ingawa hakuna idadi kamili ya watu waliouliwa wakati wa utawala wa Idi Amin kuanzia mwaka 1971-1979, inakadiriwa kuwa watu 500,000 waliuliwa wakati huo.
Mary Karoro Okurut, msemaji wa chama tawala cha Uganda akizungumzia kauli hiyo ya Chavez alisema kuwa mtu yoyote anayedhania kuwa Idi Amin alikuwa ni mtu mwema atakuwa na matatizo ya akili.
“Idi Amin alikuwa ni mtu mkatili ambaye aliua raia wengi wa Uganda na kisha kukimbilia nje ya nchi. Mtu yeyote anayemtetea Amin atakuwa na matatizo”.
Naye sekretari wa rais Yoweri Museveni, Tamale Mirundi, alielezea rekodi ya Idi Amin ya kuwaua wapinzani wake akiwemo mmoja wa wake zake.
“Kama unamuoa mwanamke na kisha baadae unamuua, huwezi kuitwa mume mzuri”, alisema na kuongeza “Hivyo ndivyo alivyofanya Amin, aliwaua raia wengi wa Uganda hawezi kuitwa mtetezi wa nchi”.
Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na Idi Amin baadhi ya watu wakiamini kuwa ukatili anaotuhumiwa kuufanya zilikuwa ni propaganda za kumchafua huku watu wengi wakiendelea kuamini kuwa Idi Amin ndiye mhusika mkuu kwa mauaji ya watu 500,000.
Miongoni mwa mambo ya kikatili ambayo Idi Amin anatuhumiwa kuyafanya ni kuwaua watu na kula nyama zao na kuhifadhi nyama za watu kwenye majokofu.
Maafisa wa serikali ya Uganda hawajasema chochote kama watachukua hatua zozote za kidiplomasia dhidi ya Venezuela.
1. Anatajwa kuwa miongoni mwa marais madikteta na katili kuwahi kutokea katika uso wa dunia.
1. Aliwahi kuwa bingwa wa ndondi wa uzito wa juu nchini Uganda mwaka 1960-1961
2. Alijichagua kuwa Raisi wa Uganda kwa mapinduzi ya kijeshi, na waganda wengi walimchukulia kuwa ni shujaa kwa kumuondoa raisi walieona “anasuasua” Milton Obote mwaka 1971.
3. Idadi ya watu waliouawa Uganda kutokana na utawala wake imekadiriwa kuwa kati ya 100,000 na 500,000 kwa kipindi cha miaka 8 aliyokuwepo madarakani kabla ya Kung’olewa na Majeshi ya Kitanzania mwaka 1979 baada ya kutaka kuteka sehemu ya Tanzania.
4. Aliwatimua raia wote wenye asili ya Kihindi nchini kwake na kutaifisha mali zao zote.
5. Alijipa vyeo kibao na kujiita Field Marshall Al Hadj Doctor Idi Amin Dada!
6. Inasemekana alimtumia Malkia wa Uingereza Elizibeth II barua za kimapenzi akimuomba amuoe ili aweze kujiita mfalme kwani alikuwa ameshajipa vyeo vyote kasoro “King” Yaani mfalme.
7. Ana watoto zaidi ya 40 huku akiwa ameoa wake 6. Mmoja wa wake zake alikutwa ameuawa kinyama baada ya kupata ujauzito na mtu mwingine.
8. Vyombo kadhaa vya habari vimekuwa vikimuhusisha na ulaji wa nyama za watu hasa maadui zake aliowaua.
9. Licha ya Ukatili dhidi ya binadamu, Idi Amin hajawahi kufikishwa mahakamani mpaka anakufa mwaka 2003 na kuzikwa nchini Saudi Arabia alikokuwa akiishi uhamishoni.
10. Aliwahi kutua Nairobi kwa dharula na akiwa na mahusiano mabaya na nchi ya Kenya, Ndege yake ilibainika kuwa na hitilafu serikali ya Kenya ilimpatia Ndege ya Polisi ili imfikishe Kampala lakini Alikataa kuhofiwa kutungulia hivyo kupelekea Makamu wa Rais wa kenya kupanda nae mpaka Kampala