Man Kush "Usikuje kanisa yangu kama huna pesa"



Mtumishi wa Mungu namcheshi Man Kush amesema kwamba hataki watu ambao hawana hela katika kanisa lake.


Akizungumza na kituo kimoja cha habari, Kush amesema kuwa wakristu wengi wanakwenda kanisani kuombewa ili wapate pesa badala ya kujituma katika mishe tofauti kutafuta riziki.

Mhubiri huyo amekiri kwamba sehemu lilipo kanisa lake, Kuna biashara ya kinyozi na sehemu za burudani ambazo hazihusiki kabisa na mambo ya kidini. Ameongezea kwamba imani ya mtuni ya muhimu zaidi kuliko kunakojengwa na kufanyiwa ibada.

Kuhusu yeye kuathirika na janga la Corona, Man Kush amesema kwamba maisha yake yanaendelea vizuri kabisa kwa sababu haendi kanisani kutafuta pesa na kwamba ana Mambo mengine tofauti ambayo yanamuingizia kipato.

"Mimi siendi kutafuta pesa kanisani, niko na mambo yangu ninafanya,"Man Kush alisema.


Amewarai wahubiri kukoma kuwatumia wakristu kujitajirisha na badala yake kuwaambia ukweli kuhusu jinsi wanaweza kujenga maisha mazuri ya baadaye.

Aidha amesema kwamba kitu cha pekee ambacho kinaweza kikamnyima raha ni kukosa hewa ya kupumua na mke wake kutomsalimia asubuhi, huku akiongezea kuwa mwanamke mzuri hapatikani kanisani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad