Si mnajua wanyonge walifundishwa kuchukia hawa watu.
Guys, mimi sio mtetezi wa hawa watu na mnanijua nishamsemaga sana Ridhwani ila c’mon, he deserves the chance to prove himself.
Point ya kutokumkubali mtu eti sababu baba yake alikuwa Rais kwa hiyo yeye asiwe ni kukosea sana.
Inabidi tuelewe kuwa watoto siku zooote wako inspired na wazazi wao. Sasa huyu Ridhwani toka yuko tumboni kwa mamake hakuna anachokijua zaidi ya siasa kweli mlidhani atakuja kuwa nani kama sio mwanasiasa?
Tum discount kwa facts labda tuseme fisadi etc ila sio tuseme hafai sababu babake alishakuwa Rais.
Marekani ni moja ya nchi inayoheshimu demokrasia kupita maelezo ila walishakuwa na Rais Baba (Bush), akaja Rais mtoto mtu ( George Bush) na hii juzi kama isingekuwa Trump kugombea Urais ilibaki kidunchu tupate tena Rais kutoka familia ya Bush.
Sasa kama marekani wameshindwa kuzuia familia moja kuongoza nchi sababu wanaheshimu demokrasia sisi tutaweza? Cha msingi tuwe na facts za kutokumtaka mtu.
Hongera Ridhwani. Ila una deni kubwa na watanzania, ile sheria ya mitandao. Wewe na January mliplay a huge part ile sheria kupitishwa. Na umeona how ile sheria ilitumika kuumiza watanzania miaka mitano hii. Sasa tunakuomba ufanyie marekebisho ile sheria…..
Cha pili kabisaaaaaaaa, Lukuvi tulikuwa tunalia nae issue ya madalali kuwa kero kubwa kwa wananchi wanaopanga. Na Lukuvi alitoa tamko kuwa madalali wasiwadai wapangaji kodi ya mwezi mmoja wawe wanalipwa na mwenye nyumba. Ila lile tamko halijafanyiwa kazi wananchi wa Mama Samia bado wanalia. Sasa tunakuomba sana sana hii ndo iwe project yako ya kwanza kabisa.
Trust me watanzania hawatosahau kama ukiwasaidia kwenye hili.