TAARIFA!
SIO MIMI - Awali ya yote ningependa kuwapa pole familia yangu, mashabiki, wafanyakazi wenzangu na wadau wangu kwa mshtuko wowote waliopata kutokana na kadhia hii. Kuna video ya utupu inasambazwa mitandaoni (inaonyesha msichana anayefanana na mimi) na kuhusisha jina langu. Mimi Meena Ally, ningependa kuwataarifu Watanzania wenzangu kuwa msichana aliyeko kwenye video hiyo SIO MIMI na sihusiki kabisa na maudhui hayo ni mtu/watu walioisambaza na kuandika jina langu.
Kama raia, mfanyakazi na mdau wa kazi mbali mbali naheshimu sheria ya nchi, brand yangu na muhimu zaidi utu wangu.
Ninaandika haya kwa sababu si tu nafananishwa na msichana alie katika video hiyo, bali pia kuna mahali kwenye video hiyo imeandikwa jina langu.
Nawasihi Watanzania wenzangu wasihusike katika kuisambaza hii video zaidi kwani tayari nimeshaifungulia kesi na upelelezi unaendelea kumtafuta aliyeisambaza na kuihusisha na jina langu na kampuni ninayofanya kazi @cloudsfmtz
Nichukue nafasi hii pia kukemea vikali vitendo hivi vya udhalilishaji mtandaoni ambayo ni kinyume na sheria za nchi na utu wa binadamu. Sina shaka tutashirikiana na mamlaka husika kukamata wote waliohusika na kitendo hichi. 🙏