Maskini...Mawakili Wamkimbia R Kelly


R. Kelly ameanza kutafuta mawakili wengine wa kumuwakilisha kwenye kesi yake mjini Chicago baada ya mawakili wake wawili Steve Greenberg na Michael Leonard kuomba kuondolewa kwenye kesi hio toka June mwaka jana wakati wana mwakilisha R Kelly kwenye kesi yake iliyokuwa na makosa 14 mjini New York ambayo R Kelly alikutwa na hatia na anaweza kupewa kifungo cha maisha jela.

Kwenye kesi hii ya mjini Chicago R Kelly anakabiliwa na makosa ya kutengeneza filamu za ngono na watoto wenye umri chini ya miaka 18, Vitisho kwa mashahidi na kujaribu kununua ukimya wao. Kesi ya Chicago itaanza kusikilizwa March mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad