Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Hamad Masauni akizungumza na makamshna wa Polisi nchini
WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Hamad Masauni ameitisha kikao cha watendaji wakuu wa jeshi la Polisi nchini humo ili kupokea na kujadili jinsi ya kudhibiti matukio ya mauaji ya kijamii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Aidha, Masauni amewataka Polisi kuwasaka na kuwakamata wanaosambaza picha chafu mitandaoni, wanaochafua viongozi na wanaosajilia watu laini za simu.
Masauni ametangaza adhima hiyo leo Jumamosi, tarehe 29 Januari 2022, alipotembelea Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) jijini Dar es Salaam.
Masauni aliyepanda wadhifa na kuwa wiziri wa wizara hiyohiyo hivi karibuni kwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ameitisha kikao hicho, ofisini kwake jijini Dodoma keshokutwa- Jumatatu tarehe 31 Januari 2022.
Waziri huyo ametoa ameitisha kikao hicho ikiwa ni siku nne, tangu Makamu wa Rais wa Tanza ia, Dk. Philip Mpango kutoa siku saba kwa Inspekta Jenerali wa Polisi – IGP Simon Sirro kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya mauaji pamoja na kukomesha matukio hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Hamad Masauni
Dk. Mpango alitoa agizo hil tarehe 26 Januari, 2022 alipotembelea wafiwa wa ndugu wa marehemu watano wa familia moja waliofungiwa ndani na kuuawa, lilitokea hivi karibuni katika kijiji cha Zanka wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma.
“Nimefika hapa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kuja kutoa pole kwa familia ambayo imetendewa ukatili huu, lakini kutoa pole kwa kijiji cha Zanka na vijiji vyote vya jirani… poleni sana.
Makamu huyo wa Rais alisema,”Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, nifikishie salam kwa IGP, mauaji haya nchi nzima yakome, mfanye kazi ya kuyazuia, polisi mna kazi kubwa ya kufanya nchini. Rais Samia na mimi tumechoka hatuwezi kuongoza nchi yenye mauaji namna hii.”
Maagizo hayo ya Dk. Mpango anayatoa kipindi ambacho kumekuwapo na ongezeko la mauaji ya wananchi ama kunyongwa, kujinyonga na au kuuawa katika maeneo mbalimbali.