Mbosso Hana Kiki Hapa Mjini Wala Skendo za Ovyo Ila Nyimbo zake ni Kubwa




Baada ya @mbosso_ kuingia Wasafi watu wengi walikuwa na mashaka juu ya uwezo wake, walijua uwezo utashuka sana maana Alipotoka Yamoto band alikuwa wamoto, lakini baada ya kuingia wasafi moto ukazidi kuwaka wala haukuzima kama baadhi ya watu walivyotegemea.

Hivi sasa mbosso ni mwanamuziki mkubwa sana nchini Tanzania, mafanikio yake ya muziki hayategemei attention, kiki, mademu na skendo, bali ni uwezo wake binafsi, inshort huyu jamaa muziki wake unaongelewa zaidi kuliko maisha yake.

Baada ya kuachia album yake "Definition of Love" kila mtu aliyeisikiliza kwa makini alikubali uwezo wa mbosso, mbosso hacopy na kupaste, analadha yake ya kipekee na hakuna ambaye anaweza kuiga uimbaji wake.

Mbosso ni mtaalamu wa mashairi hasa ya mapenzi, hilo limefanya apate jina jipya la mbossokhan, jina hili limekuja baada ya watanzania kuanza kumfananisha na Wahindi katika sekta ya mapenzi.

Mbosso ni moja ya wasanii wanaofanya vizuri youtube na Digital platforms kubwa Africa na Dunia kwa ujumla.

Mbosso ni msanii muhimu sana pale wasafi kwani anapeperusha bendera yao vizuri, ndani na nje ya Tanzania.

Kupitia mbosso, wanamuziki inabidi wajifunze kwamba kutumia kiki na skendo za hovyo hovyo sio njia nzuri kutoboa kimuziki, unaweza kutoboa kupitia kipaji chako tu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad