Mbunge mmoja wa zamani wa Hong Kong amefungwa jela leo kwa kufichua uchunguzi wa ufisadi kuhusu jinsi afisa mmoja mwandamizi wa polisi alivyoshughulikia kuvamiwa na kundi la watu kwa waandamanaji waliokuwa wanapigania demokrasia mwaka 2019.
Lam Cheuk-ting amepatikana na hatia ya madai matatu ambapo alifichua kuwa afisa huyo Yau Nai-keung alikuwa anachunguzwa na Tume Huru ya Kupambana na Ufisadi ICAC.
Sheria ya Hong Kong hairuhusu kufichuliwa kwa jina la mtu yeyote anayechunguzwa na tume ya ufisadi.
Hakimu Jacky Ip amempa Lam kifungo cha miezi minne jela akisema ametishia uchunguzi na usalama wa umma. Lam ambaye amekanusha yote hayo amesema atakata rufaa kutokana na uamuzi huo.